Tuesday, September 23, 2008

BREAKING NEWS: WANAFUNZI 'TISA' WAULIWA KWA RISASI

(Magari ya usalama yaliyowasili punde kukabiliana na muuaji)

Habari za hivi punde tu.Mwanafunzi anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 amevamia Chuo chake cha ufundi na kuua wanafunzi tisa ,kujeruhi vibaya wawili na wengine wakiachwa majeruhi.Muuaji huyo alijipiga pia risasi ingawa bado yupo hai.

Mwaka jana mwanafunzi mwanafunzi Pekka-Eric Auvinen(18) alivamia shule kwao na kuua wanafunzi na wafanyakazi nane.

Sheria za hapa Ufini mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 anaruhusiwa kumiliki siraha.Kitu kinachopelekea nchi ya FINLAND kuwa ya tatu duniani kwa wananchi wake kumiliki siraha huku USA na Yemen zikiongoza.

Binafsi natoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao.Najua ni kipindi kigumu kwao.

Naomba mwenyezi Mungu awape moyo wa ujasiri na uvumilivu.

Roho za marehemu wapumzike kwa Amani.Amina

Habari zaidi soma BBC

3 comments:

Kibunango said...

Naona sasa wameshatimia kumi na moja...

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yaani kamanda Kibunago ni soo.

Hii nchi siielewi.Chini ya miaka 18 haruhusiwi kununua sigara wala pombe.Ila anaruhusiwa kununu Bunduki.

Tutafika tu

Yasinta Ngonyani said...

eeh mita kullo! jamani watu kuua hawaone shida na hii inaambatana na kunywa pombe nyingi pia madawa ya kulevya. Pia nadhani wengi wanakuwa na kichaa, binafsi ninependa waangalia kwanza kama ni salama kabla hawajaanza kumiliki silaha.Marehemu wastarehe kwa amani