Dada Emma Palonen ni mtanzania mbaye anaishi hapa Tampere.Nimekuta leo picha yake kwenye bango akiwa ni mmoja wa wagombea udiwani katika manispaa ya Tampere.
Binafsi nilifarijika kwanza,namfahamu binafsi kama ni dada mchapakazi,anajiamini na anauwezo mzuri wa kujenga hoja.
Nilipo ona picha yake kwenye bango nilitaka kumtafuta kupata 'mawili matatu' kuhusu yenye kwenye ulingo wa siasa lakini muda ukawa haruhusu.Ila nitamtafuta na kuwaletea mahojiano naye.
Dada Emma anagombea nafasi ya udiwani kupitia Chama cha Christian Democrats.
Kwa mfumo wa hapa unachagua namba ya mgombea umtakaye.
Hivyo kwa wakazi wa Tampere wenye sifa za kupiga kura unaweza kusoma kwa kubofya HAPA.
Tujitokeze kesho tarehe 26 october,2008 chagua number 107
Kila la kheri dada Emma nakuombea ufanikiwe katika uchaguzi.Tupo pamoja.
Umeanzisha Safari..naamini ..TUTAFIKA TU.
11 comments:
ni habari njema sana ..
ndio maana nawaambia wanakina dada wenzangu tunaweza mambo mengii sio tukalie tu kusubiria kila kitu cha upendeleo
.
Hongeera dada Emmma
safi edo naona siku hizi umeikumbuka blog yako baab kubwa
Jane,spain
Tatizo wakinadada au wanawake wengi hivi kwanini hatupendani?Maana usishangae hapo finland unaweza kuna wakinadada kibao wenye sifa za kupigakura ila kwa wivu utakuta watamnyima mwanamke mwenzetu na kuwapa hao wakina mc cain wa finland
Hongera kila la kheri.
Ningekuwa huko hakika kura yangu ingekuwa yako.
Masai vipi mbona wewe ukugombea?aaaa aaaa
salam kwa wote huko kamanda
Vipi mbona ujatuwekea picha za FFU finland wakitoa ulinzi kwenye kampeni za huku?
si unajua huku kwetu uchaguzi lazima FFU ..mabomu ya machozi..
Anony ...October 26, 2008 3:15 AM
umenichekesha sana ...
ila kweli vipi huko kama Chadema na CCM wanatumia Chopa..helkopta vipi huko wanatumia KLM nini?
HOJA, SAUT
Huyo dada kaenda kuweka tu CV lakini wazungu walivyo wabaguzi tena nchi zenu hizo ambazo hazina hata askari mweusi..msahau ..
ila poa bora ajaribu
Emma all the best my sister..
utashinda..nimependa sana ulivyoamua kujiamini.
nami pia nasema hongera sana dada Emma. huko ndio kujiamini
hongera Dada stand there u are nakupongeza kwa hilo.
Edo siku hizi umekuwa na spid sana nakupongeza kwa hilo!kaza buti tupe mambo mazuri!
Asante sana Matty najaribu kasafari asante sana kwa kunitembelea na wenghine wote mnaotembelea ila muda haujatosha kwenu kuacha maoni..
nawapenda wote..asanteni
Vp Matokeo ya huyo mdada?
Post a Comment