

Tamasha kubwa kabisa katika msimu wa kabaridi "AFRICA WINTER JAM FESTIVAL" litafanyika katika jiji la Tampere February 7,2008.
Tamasha litakuwa na msisimko mkubwa kwa kuleta MAGWIJI wa tasnia ya SANAA.
AFRICA NGOMA,kundi la watanzania lenye makazi yake Ujerumani litakuwepo kuleta burudani chini ya uongozi wa Ras Makunja.Ukitaka kusikia kazi zao bonyeza HAPA.
Mkongwe wa muziki wa reggae JAH KIMBUTE naye atakuwepo katika kuhakikisha TAMASHA linakuwa gumzo.Kimbute ambaye bado mashabi wake wanamkumbuka kwa 'show' kali alizowahi kuzifanya kwenye ukanda wa scandnavia.
Kubwa ya yote Mwanadada Tabia Mwanjelwa atapanda kuendeleza libeneke baada ya ukimya wa muda mrefu.
Maelezo kwa mujibu wa muandaaji wa Tamasha hilo bwana Menard Mponda.
Binafsi naamini Tamasha litakuwa baaaab kubwa..kwani kwa tuliohudhuria Tamasha la mwisho mambo yalikuwa mswano...kazi nzuri Mponda endeleza libeneke.
3 comments:
kazi nzuri..i wish ningekuwapo..nawapenda sana ngoma africa nilishwahi kuhudhuria show yao moja hapa German
salam Finland
Jane
Hao jamaa inabidi Edo muwashtue waje hadi sweden.
Inaonekana ni wakali sana kama alivyosema Jane
Ni kweli kama msemavyo wadau.Binafsi nawaafahamu kwa muda nilikuwa nasikiliza sana nyimbo zao kwenye MYSPACE.COM.
Hususani wanapojitahidi kuendelea kuhifadhi nyimbo zetu hata zile za utotoni ili historia isipotee na pia wanajitahidi kupambana na Rushwa.
Itakuwa show nzuri sana nakuhakikishia watu wangu.
Post a Comment