Thursday, May 21, 2009

Unakumbuka: MIAKA 13 AJALI YA MV BUKOBA


Mv Bukoba baada ya kugeuka chini juu.Hiyo sehemu yenye rangi nyeusi ni sehemu ambayo kawaida inakuwa chini ya maji .Walikuja watu(bila kujua wanafanya nini) walikata sehemu hiyo mbele chini yenye "ombwe" na kufanya kama pulizo lililotobolewa na meli ikazidi kuzama

Hili ni bango lilipo kwenye makaburi ya pamoja yaliyopo Igoma jiji Mwanza.Kutokana na miili ya walio wengi kuharibika na maji na hivyo kushindwa kutambuliwa na sababu zingine ilipelekea wapendwa wetu wapumzishwe kwenye makazi yao ya kudumu hapo.

Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya Mv Bukoba,wenye orodha yabaadhi ya majina ya waanga wa ajali.Nilisimama eneo hilo siku ya tukio na kuweza kuona kwa mbali eneo ambalo ajali ilikuwa imetokea tukiwa na watu wengine.Mnara umejengwa kwenye shule ya wasicha Bwiru.

Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.


Poleni sana wafiwa..tupo pamoja ..mwenyezi Mungu awapumzishe mahala pema peponi woote waliotangulia mbele ya haki.Amina

Tutafika tu

NB:Mtundiko huu utabaki mpaka jumamosi ikiwa ni njia moja ya kuomboleza.RIP



11 comments:

Anonymous said...

mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.

Nakumbuka rafiki yangu Catherine alikuwa ndio kamaliza shule alikuwa anasoma shule ya wasichana Rugabwa.Ndio alikuwa anarejea nyumbani baada ya shule.Wanafunzi karibu wote wa darasa lao walifariki.

Huzuni zaidi nilikosa hata kuuona mwili wake.Tulikutana na familia yao na kumfanyia ibada ya familia kando ya ziwa victoria.

Bado nakukumbuka wajina..Mwenyezi Mungu akuweke mahala pema.Miss'g u..an love

Anonymous said...

yaani miaka 13 tangu itokee ajali na serikali iliunda tume mwisho wa siku mpaka leo hawajatupa hata matokeo rasmi nini kilikuwa chanzo cha ajali.

tumekalia sifa za kijinga tu..mara rais wetu amekuwa wakwanza kwenda usa kumsalimia Obama..sasa inasidia nini bibi yangu singida?

ona obama anaenda july Ghana sasa wao wasemeje?

RIP ...poleni wafiwa msiba wa kitaifa

Yasinta Ngonyani said...

kweli miaka inaenda haraka kweli. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Ameni

na priscus buretta, Rombo, Keni said...

poleni, hiyo idadi ya watu waliokufa, katika hiyo ajali ya MV Bukoba inatisha sana, niliwahi safiri na meli hiyo mara nyingi sana. cha kushangaza na kusikitisha ni kuwa ajali itokee maili moja na nusu kabla ya kufika, inatia ugumu kukubaliana na hoja ya kuwa ilikuwa overloaded. lakini cha kushangaza zaidi ni kuwa hakuna ripoti juu ya chanzo cha ajali hiyo. after 12 years we may as well give up to the report. i think it was a terrible tragedy na Mungu apumzishe mioyo ya watu hao mahali pema peponi, walipitia njia ngumu mno.

Mzee wa Changamoto said...

Kuna wakati unajiuliza kama kuna namna unayoweza kuwa msaada kwa nchi na unabaki kughadhibika. Mfano ni huu upande wa uwajibikaji. Hakuna anayewajibika kwa makosa wafanyayo. Mfano ni huyo aliyeamuru kutoboa meli na kusababisha muda mfupi zaidi wa kufikiria namna ya kuokoa watu. Na kwa tetesi ni kuwa hakuwa mtu mwenye utaalamu wa meli, bali kiongozi wa kisiasa. Hakuna awazaye juu ya waliokufa, hakuna anayewatetea walioathirika na hakuna anayelitetea taifa kwa kuonesha mfano wa kuelekea kwenye usalama zaidi katika usafiri wa majini.
Kuna mengi ya kusema, kuna mengi ya kufanya na mengi ya kubadili kwa TANZANIA YANGU NIIPENDAYO
Ulalo mnono na wenye amani kwa waliotutoka

EDWIN NDAKI (EDO) said...

kweli mzee wa Changamoto tuna kabiliwa na changamoto kibao katika mageuzi ya kimaisha yetu.

mumyhery said...

we acha tu ndugu yangu mwaka 1992 niliipanda nikiwa natoka holiday Uganda nikapitia bukoba, yaani ilivyo kuwa imejaza yaani ulikuwa inaenda upande upande, yaani tulikuwa kama tunaingia kama kwenye dala dala hata ticket nilikuwa sijui zinakatwa vipi ila kwa kuwa tulikuwa na mdogo wangu aliyekuwa anaishi mwanza nafiri yeye alikuwa anajua utaratibu ila mimi nilishtukia nimepata room yaani we acha tu

lugengep said...

ajali haima kinga mungu azilaze mahala pema peponi roho za marehemu

lugengep said...

mungu azilaze mahali pema roho za marehem

saadam said...

tukiangalia uzembe uliofanyika ktk ajali ya mv bukoba tutaona ni kama huu uliotokea juzi, kwa mv islander na viongozi waendelea kuchunguza mpaka miaka 20 na zaidi bila ya jibu.

Anonymous said...

May God rest them in heaven.its so sad to see the government or the shipping authority neglect the safety standards of Velssels. I happened to be on board as passenger the MV bukoba four years ago. Trained as marine engineer, during my journey I had opotunity to observe the conduct of loading the ship from luggages to passengers.visited the engine room as well.its so scary. I could not sleep till the end of the journey.Had the passengers knew the misconduct of safety standerds, no body would have been on board the ship.the following are what i discovered
1.On the boarding gate there were no system in place to prove the legitimacy of the ticket.
2.any crue member has got an access to let unticked passenger on board hence make money for themselves
3.there was no scale to weigh passengers luggages getting on board.meaning there no proper systems in place that will enable the ship to carry according her capacity.
3.I was charged the so claimed to be access luggage as I boarded off the ship by looking and estimating the weight with no scale.this is pure corruption.
4. WORSE:in the engine room the ship balance is checked by pouring water on the floor.
Please. I kindly request who ever reading and has got Outhority, please do something.we can't wait until there is tragedy.think of innocent, a layman people who knows nothing.