Monday, November 30, 2009

HONGERA BLOG YA KAMALA MIAKA 3!!!

Kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa

Nina kila sababu ya kumpongeza rafiki yangu katika tasnia ya kublog Kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa kutimiza miaka 3 leo.

Kwa ambao wanablog naamini wanatambua jinsi ilivyo kazi ngumu na pia kazi nzuri kublog.Nakumbuka marafiki zangu tulioanza nao kublog leo wameamua kupumzika kuandika.

Sijawahi kukutana ana kwa ana na bw Kamala ila tumekuwa tukikutana kwa takribani miaka mitatu kupitia blog mbalimbali hasa kule kwa bwana Majid Mjengwa

Nilifurahi sana baada ya kamala kuanzisha blog yake kwa kile alichoamini kumuwezesha kupata jukwaa huru zaidi kuandika anachotaka.Hatimaye alitimiza lengo.

Nakumbuka wapo walioamini asingeweza kwenda mbali,lakini leo miaka 3 yupo kwenye libeneke.

Nakutakia kila jema katika mchakato mzima wa kublog ndugu yangu Kamala.

Unaweza kumtembelea Kamala kwa kubofya www.kamalaluta.blogspot.com

Tutafika tu.


6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

epibesidei blog ya Kamala

John Mwaipopo said...

kamala kumbe ni 'dogo' kwenye tasnia hii ya kublog. kazi ya bila kulipwa isipokuwa kufurahi na kujifunza kutoka kwa wasomaji na wachangiaji. huyu jamaa huwa napenda misimamo yake katika michango yake.

'ongela'kamala kwa blogu yako kuzidi kuchengua na machenguzi yako

mumyhery said...

Hongera sana Mkuu kwa yote tuliyopata, pia tunasubiri kwa hamu yajayo. Shukran

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Asanteni Nyoote na Edo kwa pongezi zenu, changamoto pia zinakaribishwa

Simon Kitururu said...

Hongera komandoo!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Edo
Kwa niaba ya familia yangu na wapenda mema wote nakutakia kila lililo jema wakati huu wa sikukuu na usalama kuelekea mwaka mpya
Baraka kwako